Nyimbo Za Sifa
Wimbo 174 Ewe jehova,Watwona. Maneno ya wimbo
Ewe jehova, watwona
Tumekukubali
Mjalie huyu mwana
Kuvyawa kwa pili
Kwa asili ni mbaya
Ila mkubali
Kundini mwa wako pia
Apate pahali
Msafi kwa Roho yako
Awe na urathi
Hata ufalmeni mwako
Mungu, akurithi
Aishipo hapa chini
Asione haya
Kuiungama imani
Na kukutetea
Kubali kutusikia
Hilo tukwombalo
Kwa kuwa anatwombea
Bwana jesu lilo