Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 172 Baba tunakwomba sasa. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 172 Baba tunakwomba sasa. Maneno ya wimbo

 

Baba, tunakwomba sana
Lete baraka yako
Wabarikie vijana
Tuwaletao kwako
Wawe na uthubutifu
Kama jusufu kale
Wawe na waaminifu
Kama Daudi vile

Mwokozi Mtakatifu
Ulikuwa Kijana
Ukawa myenyekevu
Mwenye kutii sana
Waongoze hawa wana
Wawe mfano wako
Hao ni wanyonge sana
Wana-kondoo wako

Ewe Roho, waongoze
Watangulie mbele
Wape amani, watuze
Wape furaha tele
Ewe Roho, wawe wako
Uwakae myoyoni
Waonyeshe nuru zako
Hata kwako mbinguni

Exit mobile version