Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 171 Ewe Baba kubali kuwabarikia Hawa Watoto wako. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 171 Ewe Baba kubali kuwabarikia Hawa Watoto wako. Maneno ya wimbo

 

Ewe Baba kubali
Kuwabarikia
Hawa watoto wako
Tukikuletea
Wape tabla mpya
Uwarejezee
Sura zako halisi
Uwakubalie

Bwana jesu zamani
Ulipenda wana
Uhwakaribisha
Waje kwako sana
Watoco hawa nao
Waliobatizwa
Wawe, Wewe na wao
Viungo na Kichwa

Roho Mtakatifu
Walinde daima
Hata mwisho ambapo
Vita vitakoma
Warejeze kipawa
Chako upya tena
Hata kwako mbinguni
Wafike salama

Baba, Mwana na Roho
Hekima, uweza
Na mapenzi watoto
Tumewabatiza
Kwa jina la Utatu
Wape raha tele
Watakase, ni wako
Walinde milele

Exit mobile version