Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 169 Sistahili mezani kuwako. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 169 Sistahili mezani kuwako. Maneno ya wimbo

 

Sistahili mezani kuwako
Hata kuzoa viangukavyo
Waniita mwenye dhambi, kwako
Siji ila kwa uniitavyo

Sistahili hata kwitwa mwana
Wala kuketi papo mezani
Nimekosa, nimetanga sana
Nisamehe, Bwana naamini

Neno moja, Bwana, Iitacosha
Uso wako likining’aria
Hapo kweli utaniwezesha
Duniani niandame njia

Ni wenye rehema moyo wako
Na ya pendo isiyopimika
Nao ndio utukufu wako
Kuinua aliyeanguka

Nasikia kuwa waniita
Naja inama, nashika miguu
Na nisiyefaa waniacha
Nikujie na uchafu huu

Sifa zangu na kuomba kwangu
Vipae daima mbele zako
Ukae, Bwana, moyoni mwangu
Nami milele nikae kwako

Exit mobile version