Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 167 Sasa Baba, tena twakumbuka. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 167 Sasa Baba, tena twakumbuka. Maneno ya wimbo

 

Sasa Baba tena twakumbuka
Hayo mapenzi yaliyo makuu
Na kwa hayo sisi twaokoka
Ukombozi wa mara moja tu
Ni Bwana kutufia Mtini
Sisi tuiiokuwa dhambini

Mwangalie, Baba, uso wake
Makosa yetu usitwonee
Ukatwangalie ndani yake
TwamtakaYeye atwombee
Kati ya dhamba zetu na Wewe
Tuna Bwana na mateso yake

Twaungama, mambo ya dunia
Yaiharibu imani yetu
Nguvu zako hatukutumia
Zalegea mno sala zetu
Tunastahili na adhabu kuu
Twatumaini kwako Bwana tu.

Twawaombea wapenzi kwako
Kwa jina lake Bwana jesu tu
Waambate kifuani mwako
Watende kwa rehema zako tu
Walinde, wawe sa?, weupe
Na nguvu za kwendelea wape

Basi twaja, miguuni pako
Ewe Mwokozi mvumilivu
Twazitegemea pendo zako
Tupe wokofu mtimilivu
Kazini mwako tufurahiwe
Na milele tusitengwe nawe

Exit mobile version