Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 165 Njoni Karamuni. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 165 Njoni Karamuni. Maneno ya wimbo

 

Njoni karamuni
Mmeitwa
Vyakula mezani
Vimewekwa
Na mwaka nyumbani
Mlazwe rahani
Mwake kifuani
Njoni, njoni

Mkate wakweli
Ametoa
Wa bure, si ghali
Utapewa
Wote awaita
Wengi wamepata
Nanyi awavuta
Njoni, njoni

Njoni kulingana
Mungu Bwana
Mwambieni kila
Haja tena
Mtakavyo vyote
Hupa siku zote
Neema kwa wote
Njoni, njoni

jesu, twaja wako
Tukubali
Pia tuwe wako
Safi kweli
Kisho huko juu
Penye enzi kuu
Tutaziimba tu
Sifa zako

Exit mobile version