Nyimbo Za Sifa
Wimbo 164 Mungu wangu, Meza Yako. Maneno ya wimbo
Mungu wangu, meza yako
lmeandikwa tayari
Ongoza watoto wako
Waje kula, wafurahi
Kikombe cha pendo zako
Kotekote chamwagika
Watu wako wanywe hizo
Zi tamu, zina baraka
jesus ametuletea
Baraka, mwili na damu
Karamuni twaingia
Tukale yetu sehemu
Wengine wamekataa
Hawatupenda wenyewe
Ila Jesus awafaa
Yeye hakatai kamwe
Wengine wapenda dhambi
Waonea mwito wake
Kwa dhambi wewe hushibi
Sidharau kifo chake
Ni karamu takatifu
Na wawe wengine wageni
Wote wapate wokofu
Wajao hapa mezani