Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 163 Ni Mfalme wa Mapenzi. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 163 Ni Mfalme wa Mapenzi. Maneno ya wimbo

 

Ni Mfalme wa mapenzi
Ndiye anichungaye
Sipungukiwi, hawezi
KunipotezaYeye

Kando ya maji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisha mema
Daima hunilaza

Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu
Naye huniandamia
Hunirudisha kwangu

Uvulini mwa mauti
Sichi hatari kamwe
Wewe Bwana huniachi
Mwokozi wangu Wewe

Waniandikia meza
Neema kwako tele
Kwa Wewe, yote naweza
Na Msalaba mbele

Kamwe hautapungua
Uule wema wako
Mwisho, atanichukua
juu, niimbe kwako

Exit mobile version