Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 161 Jesu furaha ya Myoyo. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 161 Jesu furaha ya Myoyo. Maneno ya wimbo

 

Jesu furaha ya myoyo
Yenye mapenzi, yaachwe
Yote yatupendezayo
Tukuzingatie Wewe

Kweli yako nda daima
Wawajibu wakwitao
Na siku zote U Mwema
Kwao wakutafutao

U mkate we Uzima
Kupokea ni baraka
Twanywa kwako, U Kisima
Roho zikiburudika

Mwokozi twakutamani
Kwako roho hutulia
Twakushika kwa imani
Nawe watubarikia

jesu, ndiwe kwetu mwanga
Tufurahishe daima
Giza ya dhambi fukuza
Uwe Mwanga wa uzima

Exit mobile version