Nyimbo Za Sifa
Wimbo 160 Hapa Nakwona Mwokozi Wangu. Maneno ya wimbo
Hapa nakwona mwokozi wangu
Kwa imani, nami nakushika
Nakutupia unyonge wangu
Kwa neema yako naokoka
Hapa nala mkate wa Mungu
Hapa nanywa divai ya mbingu
Hapa natua mzigo wangu
Hapa hufurahi roho yangu
Msaada mwingine hapana
Wala sitaki,Wewe watosha
Nakutengemea Wewe Bwana
Siku zote wanifurahisha
Ni zangu dhambi, haki ni yako
Na damu yako yanitakasa
Haki nayo nimepata kwako
Vao Ia arusi sitakosa
Vitu mezani vyaondolewa
Ila mapenzi hayaondoki
Uwapo Wewe twabarikiwa
Ngao na jua kwetu hutoki
Huku karamu nyingi zapita
Zatukumbusha hiyo ya juu
Wewe, Bwana, utakapotwita
Ni karamu ya furaha kuu