Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 159 Hata Aje ni Furaha Kukumbuka Neno Hili. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 159 Hata Aje ni Furaha Kukumbuka Neno Hili. Maneno ya wimbo

 

Hata aje ni furaha
Kukumbuka neno hili
Mbele yetu kuna raha
Muda mchache, si mbali
Mbingu, kwetu tuvingoje
Tusubiri, hata aje

Wapenzi wetu wa chini
Wakipata raha juu
Na huku tuna huzuni
Mbele ni furaha kuu
Kuwaona, na tungoje
Kuonana, hata aje

Tuna mawingu na giza
Na majonzi ya dunia
Msalaba waumiza
Ila twayavumilia
Tumefundishwa tungoje
/ya mbinguni, hata aje

Karamu imeandikwa
Mkate nao uliwe
Divai nayo tuinywe
Ili Bwana akumbukwe
Karamu juu tungoje
Tusubiri, hata aje

Twatumia haya chini
Hata Bwana atutwae
Tule hiyo ya mbinguni
Sote kwa Bwana tupae
Tungoje ili twonane
Tumetengwa, hata aje

Exit mobile version