Nyimbo Za Sifa
Wimbo 157 Bwana jesu Ndiye Atwitaye. Maneno ya wimbo
Bwana jesu ndiye atwitaye
Asema“Njoni” twendeni sote
Tukapumzike na tukae
Huku faraha, tuache yote
Najua mmechoka, dunia
Na udhia wake, havikomi
Tueni mizigo yenu pia
Mrejezwe nguvu kwangu Mimi
Njoni,’ tukapumzike hapa
Yawalemeayo nitwekeni
Baba yangu nami tutawapa
Raha isiyo ya duniani
Pumzikeni, safari hii
Ni kubwa, nayo yawaumiza
Mkate ni huu, na divai
Tumieni, mpate fuliza
Kisha endeni mbele. mfanye
Yawapasayo ya duniani
Hata Bwana aje akusanye
Watu wake rahani mbinguni