Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 156 Aleluya! Aleluya! Aleluya!. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 156 Aleluya! Aleluya! Aleluya!. Maneno ya wimbo

 

Aleluya! Aleluya! Aleluya!
Hivi vita vimekoma
Vimeshindwa na uzima
Naasifiwe daima
Bwana jesu

Nguvu za kifo ni hizo
Ila hazina uwezo
Ndizo sasa avunjazo
Bwana jesu

Siku tatu za huzuni
Kisha atoka ufuni
Asifiwe duniani
Bwana jesu

Mikufu ameivunja
Mbingu amezifungua
Nasi sasa twamwimbia
Bwana jesu

Na ulivyopigwa Wewe
Ni kwamba tufunguliwe
Milele na usifiwe
Bwana jesu

Exit mobile version