Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 154 Twimbe Wake na Waume. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 154 Twimbe Wake na Waume. Maneno ya wimbo

 

Aleluya! Aleluya! Aleluya!
Twimbe wake na waume
Ndiye wa mbingu Mfalme
Ameshinda kifo Yesu, AleIuya

Asubuhi ya Pasaka
Wanawake wakatoka
Wamwone alikowekwa, Aleluya

Hao ndio wamekaa
Malaika wamevaa
Nguo zilozozagaa, Aleluya

Wakawauliza. “Kwani
Kumtafuta ufuni
Naye yu hai, jueni,Aleluya

“Akali kwa watu wake
Kumbukeni neno lake
Ni la kufufuka kwake, Aleluya

“Nami ndimi Mwanadamu
Watu watanihukumu
Ha sikai kuzimu, AleIuya

“Kwa wanangu muwasili
Waambieni na hili
Tutaonana Galili, Aleluya

Aleluya! Aleluya! Aleluya!
Usiku waikutana
Kwa hofu, akaja Bwana
“Ni amani” akanena,Aleluya

Thoma aliposikia
Hilo aliwaambia
Ni sharti kumwangalia,Aleluya

“Ati! Thoma huzioni
jeraha za mikononi
Miguuni, ubavuni?”, Aleluya

Mara akasujudia
Kwa imani akanena
“Bwana wangu, Mungu tena!,Aleluya

Kweli wongofu ni wao
Hao waamaniao
Heri kama waonao,Aleluya

Ni siku bora ya shani
Nanyi kwa Mungu imbeni
Za sifa na shukurani,Aleluya

Exit mobile version