Nyimbo Za Sifa
Wimbo 15 Namwandama Bwana. Maneno ya wimbo
Namwandama Bwana kwa
alilonena
Njia yangu huning’azia
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.
Chorus
Amin utii, njia pweke ni hii
Yo furaha kwa Yesu: amini
ukatii
Giza sina kwangu wala hata
wingu
Yeye mara huviondoa
‘Woga, wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini nitii pia.
Masumbuko yote, sikitiko lote
Kwa mapenzi hunilipia
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki
Taamini nitii pia.
Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa
Napata fadhili na radhi kamili
Taamini nitii pia
Nitamfurahia na kumtumaini
Majumbani na njia-njia
Agizo nacenda; nikitumwa
hwenda
Huamini nitii pia.