Nyimbo Za Sifa
Wimbo 148 Siku Zetu Hwenda Mbio. Maneno ya wimbo
Siku zetu hwenda mbio
Hatujui ni lini
Tutakapokuwa nao
Walio kaburini
Yesu Mkombozi mwema
Waamshe walalao
Nao wajute mapema
Watunze njia zao
Tujue tunakokwenda
Kuna njia mbili tu
Moja yapeleka kwako
Ya pili kwa dhiki tu
Siku zenda mbio sana
Tuhifadhi,jesu Bwana
Tuii hai, au wafu
Tuwe wako pasipo hofu
Kama kivuli kilivyo
Ndivyo uzima wetu
Hivi, myaka ipitavyo
Tushinde dhambu zetu
Tuwe na akili sisi
Si wavivu kazini
Na tusishindwe na nafsi
Kuna raha mbinguni
Mbele za mwamuzi wetu
Akija aamue
Utuondolee hofu
Yesu, utuombee
Siku zenda mbio sana
Tuhifadhi, Yesu Bwana
Tuli hai, au wafu
Tuwe wako pasipo hofu