Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 147 Na Myaka Michache. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 147 Na Myaka Michache. Maneno ya wimbo

 

Na myaka michache
Hivi ipitavyo
Asipotokea Bwana
Tutapita vivyo

Nifanye tayari
Osha dhambi zangu
Nikubali siku ile
Ewe Bwana wangu

Jua nalo lina
Siku kidogo tu
Na tutakwenda ambapo
Mwana ndiye nuru

Nifanye tayari
Osha dhambi zangu
Nikubali siku ile
Ewe Bwzma wangu

Na vivyo ni chache
Siku za tufani
Hapana tufani kamwe
Twendapo mbinguni

Nifanye tayari
Osha dhambi zangu
Nikubali siku ile
Ewe Bwana wangu

Ni kwa siku chache
Kuachana kwetu
Mashindano na machozi
Hayako huko juu

Nifanye tayari
Osha dhambi zangu
Nikubali siku ile
Ewe Bwana wangu

Sabato chache tu
Twafurahi sana
Halafu Sabato ndefu
Pamoja na Bwana

Nifanye tayari
Osha dhambi zangu
Nikubali siku ile
Ewe Bwana wangu

Bado siku chache
Atarudi tena
Yeye aliyetu?a
Nasi tutamwona

Nifanye tayari
Osha dhambi zangu
Nikubali siku ile
Ewe Bwana wangu

Exit mobile version