Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 143 Wakristo walio na Furaha. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 143 Wakristo walio na Furaha. Maneno ya wimbo

 

Wakristo walio na furaha
Leo raukeni na mapema
Yesu Mwokozi wa ulimwengu
Amezaliwa, Mwana wa Mungu
Siri za mapenzi zieneze
Watu wote n wayatukuze

Ni malaika aliyenena
Aliyeleta habari kwanza
Kwao wachunga waliolinda
Kuonyesha Mungu awapenda
Huyu malaika akasema
“Nawaletea habari njema

“Leo, Mungu amelitimiza
Agano lake, hakubakiza
Mwokozi wenu amezaliwa
Yeyule aliyeahidiwa
Habari njema kwa watu wote
Taifa za duniani zote

Mara hiyo malaika wengi
Wako, pamoja, sauti nyingi
Waziimba sifa za Mapenzi
Ni Mapenzi yenye Ukombozi
“Enzi ni yake Mungu wetu juu
Kwa atu nao ihisani kuu.”

Wachunga wakaenda haraka
Alivyoyanena malaika
Waione ajabu ya Mungu
Aliyotenda kwa walimwengu
Wakamwona Mwana kihorini
Na Mama, na jusufu, bandani

Sisi na tutafakari sana
Mapenzi ya ajabu, hapana
Kama haya ya Mungu, tunzeni
Maisha ya Mwana duniani
Kuzawa, hata kaburi yake
Na sisi twandame nyayo zake

Kisha, na sisi twatumaini
Tuwe mumo jeshini, mbinguni
Tuliookoka kwa mapenzi
Tumwone huko katika enzi
Tukiona utukufu wake
Na milele twimbe sifa zake

Exit mobile version