Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 140 Uliposhuka kwa Kunitaka. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 140 Uliposhuka kwa Kunitaka. Maneno ya wimbo

 

Uliposhuka kwa kunitaka
Ukiacha enzi yako
Bethilehemu ku hali ngumu
Hapana nafasi kwako!

Njoo ukae kwangu Yesu
Moyoni nafasi iko!

Ni malaika walioimba
Ulipozaliwa huko
Ulikubali hali dhaifu
Padogo pahali pako

Njoo ukae kwangu Yesu
Moyoni nafasi iko!

Mbweha mwituni hukaa kwao
‘Nyani wako matunduni
Mwana wa Mungu si fungu lake
Hana pumziko chini

Njoo ukae kwangu Yesu
Moyoni nafasi iko!

Ukaja Bwana wawe wangwana
Kila raia wako
Wakakucheka, wakakuvika
Miiba kicwani mwako!

Njoo ukae kwangujesu
Moyoni nafasi iko!

Na malaika watakwimbia
Ukija enzini mwako
“Upesi, Bwana kuna nafasi
Kwa Baba nafasi iko!”

Tutaona furaha, Yesu
Kwitikia mwito wako

Exit mobile version