Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 14 Kumtegemea Mwokozi. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 14 Kumtegemea Mwokozi. Maneno ya wimbo

 

Kumtegemea Mwokozi
Kwangu tamu kabisa
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni

Yesu,Yesu namwamini
Nimemwona thabiti
Yesu,Yesu yu thamani
Ahadi zake kweli

Kumtegemea Mwokozi
Kwangu tamu kabisa
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili

Kumtegemea Mwokozi
Kwangu tamu kabisa
Kwako daima napata
Uzima na amani

Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea
Yesu, Mpendwa na Rafiki
Uwe nami dawamu.

Exit mobile version