Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 139 Na Twimbe Leo. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 139 Na Twimbe Leo. Maneno ya wimbo

 

Na twimbe Ieo kwa kuwa
Yesu Kristo amezawa
Tumepewa Mwana-Mungu
Aje akatue huku

Na twimbe Ieo kwa kuwa
Yesu Kristo amezawa

Ndiye Seyidi wa wote
Muumba wa vitu vyote
Amekuja duniani
Kutukomboa dhambini

Na twimbe Ieo kwa kuwa
jesu Kristo amezawa

Bwana wa mabwana wote
Jua la mianga yote
Amekubali machungu
Tuwe watoto wa Mungu

Na twimbe Ieo kwa kuwa
Yesu Kristo amezawa

Haki na salama tena
Kwetu vimeshikamana
Watu wamesamehewa
Mungu amependezewa

Na twimbe Ieo kwa kuwa
Yesu Kristo amezawa

Mungu Baba tumsifu
Naye Mwana mtukufu
Naye, Roho Mtulizi
Mungu na apewe enzi

Na twimbe Ieo kwa kuwa
jesu Kristo amezawa

Exit mobile version