Nyimbo Za Sifa
Wimbo 138 Sasa naTuimbe Wimbo. Maneno ya wimbo
Sasa na tuimbe wimbo
Ule’wa zamani
Hauna mwenziwe huo
Hapa duniani
Twambimbia Mungu wetu
Wimbo wa daima
“Sifa juu ni ya jesu,
Kwa watu salama.”
Akaja kutuhubiri
Mapenzi ya Baba
Na huruma zake kwetu
Daima si haba
Naye hutung’arizia
Nuru za uzima
“Sifa juu ni ya Yesu,
Kwa watu salama.”
Akaja kuwaletea
Wanyonge amani
Kuwaonyesha wokofu
Walio dhambini
Wakubwa, wadogo pia
Kuwatenda vyema
“Sifa juu ni ya Yesu,
Kwa watu salama.”
Akaja kutuletea
Vitu vya thamani
Alitupenda, ndiposa
Akashuka chini
Wimbo wao malaika
Na twimbe daima
“Sifa juu ni ya Yesu,
Kwa watu salama.”