Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 135 Ni Usiku wa Manane,Wachunga Wakesha. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 135 Ni Usiku wa Manane,Wachunga Wakesha. Maneno ya wimbo

 

Ni usiku wa manane
Wachunga wakesha
Mara likawatokea
Lililowastusha
Malaika wa kumeta
Awapa habari
“Amezaliwa Mwokozi
Nawapa dalili

Mara wakaja wengine
Jeshi toka mbingu
Wapaza sauti zao
Wakisifu Mungu
Waimba:“Enzi ni yake
Mungu bora Sana
Kwa watu, amani kuu
Wenye kuridhiwa!”

Waliuimba zamani
Malaika wa ajabu
Malaika wanapiga
Vyombo vya dhahabu
Waimbai“Enzi ni yake
Mungu bora sana
Kwa watu, amani kuu
Wenye kuridhiwa!”

Hata sasa huku chini
Wakali kushuka
Nao wanatuimbia
Wao malaika
Barani hata mijini
Wapaza sauti
Na kutwimbia maskini
Wao hawaachi

Wasema: “Enyi watumwa
Mmetumwa sana
Kwa kufanya kazi nzito
Huku mkiguna
Msihuzunike mno
ltakuja raha!
Pumueni mkiimba
Wimbo wa furaha

“ltakuja na upesi
Myaka mitukufu
Hivyoandikwa kale
Katika kitabu
Mbingu mpya, na dunia
Ya Mwenye amani
Nanyi mtatwitikia
Twimbao mbinguni!”

Exit mobile version