Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 130 Hapo Kale, Kama Wakati Huu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 130 Hapo Kale, Kama Wakati Huu. Maneno ya wimbo

 

Hapo kale, kama wakati huu
Wachuga walilinda kundi lao
Si nyumbani, walala barani tu
Hayo wawingu ndiyo paa Iao
Ni usiku sana, moto wawaka
Humo maragoni, wote walala
Mara mbinguni sauti yatoka
Na nchi nayo chini hunyamaa

Yuko malaika karibu nao
Utukufu Mungu unang’ara
Walikucha sana wachunga hao
Wakaficha nyuso na kunyamaa

Akasema malaika pekee
“Msiche, mimi ni mjumbe, kwenu
Nimetumwa, ili niwaletee
Habari njema ya furaha kuu

“Leo hivi katika mji huu
Wa Bethilehemu, kibandani
Amezaliwa Mfalme Mkuu
Ndiye Mwokozi Kristo wa mbinguni”

Mara, jeshi ya malaika kuu
Waimba wimbo wa furaha kuu
“Sifuni Mungu wa mbinguni juu
Kwa watu chini mapenzi makuu.”

Exit mobile version