Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 127 Msifuni, Yesu Ndiye Mkombozi. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 127 Msifuni, Yesu Ndiye Mkombozi. Maneno ya wimbo

 

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi,
Imbeni ya pendo zake kuu,
Sujuduni, malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu,
Kama vile mchunga achungavyo.
Vivyo sisi kutwa atuchunga,
Msifuni mlio wake watoto
Msifuni aliye Mchunga.

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi;
Akateswa tupate ongoka
Ndiye Mwamba, Dhamana ya kuokoka,
Sujuduni kwake Muangikwa,
Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za Baba yaka Mungu,
Aliyefyolewa na kusulibiwa,
Msifuni ndilo Ietu fungu.

Msifuni, Yesu ndiye Mkombozi;
Shindukeni, enyi milango juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu,
Atakuja kuitawala nchi,
Yesu, Mwombezi wetu wa Mungu,
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kwali Mwana wake Mungu.

Exit mobile version