Nyimbo Za Sifa
Wimbo 116 Ati Twonane Mtoni?. Maneno ya wimbo
Ati twonane mtoni’?
Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.
Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni
Mtoni! ·
Tutakutanika mtoni
Penye kiti cha Mungu.
Tukitembea mtoni
Na Yesu Mchunga wetu
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
Kwangara sana mtoni
Cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani
Tumsifu kwa nyimbo.
Si mbali sana mtoni,
Karibu tutawasili,
Mara huwa furahani
Na amani ya kweli.