Nyimbo Za Sifa
Wimbo 115 Mungu Ulisema. Maneno ya wimbo
Mungu ulisema,
Giza ilikoma;
Twashukuru!
Twakusihi sote,
Duniani mote
Na kwa watu wote
lwe nuru.
Yesu ulikuja,
Ulituletea
Nuru kuu,
Macho kwa vipofu,
Maisha kwa wafu
Nasi twakusifu,
Twashukuru.
Roho kiongozi,
Roho wa mapenzi
Tia nuru;
Mwovu hata sasa
Watu huwatosa,
Tunakwomba hasa,
Iwe nuru,
Mungu wa Utatu
Mwanga wao watu,
Tuwe huru;
Twende kote-kote
Wafundishwe wote
Dunia mote
lwe nuru.