Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 114 Nimeketi Mimi Nili Kipofu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 114 Nimeketi Mimi Nili Kipofu. Maneno ya wimbo

 

Nimeketi mimi nili kipofu
Gizani nangojea macho;
Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu,
Ondoa dhambi zangu nzito.

Huruma hakuna aoneaye.
Gizani nangojea macho.
Sasa nitakase nikuishiye
Yesu, na dhambi zangu nzito,

Tangu siku nyingi nimepofuka
Natamani uso nikwone;
Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka,
Sema nemo, basi, nipone.

Nimeketi mimi nili na giza,
Nami ya kutumai sina;
lla nasikia kunongoneza,
“Kwake Yesu kuna kupona.”

Exit mobile version