Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 113 Bwana Yesu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 113 Bwana Yesu. Maneno ya wimbo

 

Bwana Yesu, Bwana Yesu
Mbona unaumia? Unateseka sana
Kwa ajili ya kuomba
Waomba na jasho jingi Iikageuka damu

Chorus
Kumbe! ni dhambi zangu zinazokuumiza
Bwano wangu, Mungu wangu
Mimi Ieo, naja kwako
Ili niziungame

Bwana.Yesu, Bwana Yesu
Mbona unaumia na mizigo mizito?
Umejitwalia Wewe msalaba mabengani
Kwa ajili ya watu

BwanaYesu, BwanaYesu
Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi
Bila tusi ukalia, Baba wangu, wasamehe
Chukua roho yangu

BwanaYesu, Bwana Yesu
Muda ulipofikia, nchi ikawa giza
Mbinguni pakatulia, angani pakawa kimya
Watu wakaogopa

BwanaYesu, BwanaYesu
jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba
Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni
Naimba, Haleluya

Exit mobile version