Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 11 Ewe Roho wa Mbinguni. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 11 Ewe Roho wa Mbinguni. Maneno ya wimbo

 

Ewe Roho wa Mbinguni
Uje kwetu sasa
Ufanye makazi yako
Ndani ya kanisa

Ndiwe Mwanga, umulike
Tupate jikana;
Mengi kwetu yapunguka
Tujalize, Bwana

Ndiwe Moto, teketeza
Taka zetu zote;
Moyo na sadaka
Ya. Mwokozi, yote.

Ndiwe Umande, na kwako
Tutaburudika
Nchi kavu itakuwa
Ni yenye baraka

Roho wa Mbinguni uwe
Nasi hapa chini
Mwili uufananishe
Na Kichwa Mbinguni

Exit mobile version