Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 109 Tufani lnapovuma. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 109 Tufani lnapovuma. Maneno ya wimbo

 

Tufani inapovuma
Sana moyoni mwangu
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu

Chorus
Huni?cha, hunificha
Adui hatanipata
Hunificha, hunificha
Mkononi mwake

Pengine kuna taabu
Yanisongeza kwake
Naijua si hasira
Ni ya mapenzi yake

Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka

Niishipo duniani
Ni tufani daima
anilindapo rohoni
Nitakaa salama

Exit mobile version