Nyimbo Za Sifa
Wimbo 107 NilikupaWewe Maisha Yangu. Maneno ya wimbo
Nilikupa wewe
Damu ya moyoni
lliwokolewe
Winuke ufuni
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
Nilikupa miaka
Yangu duniani
Upate inuka
Kuishi Mbinguni
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
Niliacha nuru
Za Baba, Mbinguni
Kwingia taabu
Za ulimwenguni
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
Niliteswa sana
Mateso kifoni
Usije yaona
Hayo ya motoni
Nimekunyimani?
Umenipia nini?
Nimekuletea
Huku duniani
Upendo na afya
Zatoka Mbinguni
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
Nipe siku zako
Udumu mwangani
Na taabu yako
Wingie rahani
Nafsi, pendo, mali
Twae Imanweli