Nyimbo Za Sifa
Wimbo 106 Kilima Kando ya Mji. Maneno ya wimbo
Kilima kando ya mji
Alikufa Bwana
Kuokoa wakosaji
Akateswa sana
Kabisa hayasemeki
Mateso dhaifu
Alikufa Mwenye haki
Tupate wokovu
Alimwaga damu yake
Hi tuwe wema
Tufae kukaa kwake
Mbinguni daima
Hatuna mwenye imani
Aliye na haki
Wa kutosha yetu deni
Rafiki Yesu tu
Alijua peke yake
Kufungua Mbingu
Ufunguo damu yake
Kondoo wa Mungu
Aliyetupenda hivyo
Nasi tumpende
Tukamtumai vivyo
Nasi tumpende