Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 104 Mapya ni Mapenzi Hayo. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 104 Mapya ni Mapenzi Hayo. Maneno ya wimbo

 

Mapya ni mapenzi hayo
Asubuhi tuonayo
Saa za giza hulindwa
Kwa uzima kuamshwa

Kila siku, mapya pia
Rehema, wema, na afya
Wokofu, na msamaha
Mawazo mema, furaha

Tukijitahidi leo
Na mwendo utupasao
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza

Mambo yetu ya dunia
Mungu atayang’aria
Matata atageuza
Yawe kwetu ya baraka

Yaliyo madogo, haya
Mungu tukimfanyia
Yatosha: tutafaidi
Huvuta kwake zaidi

Ewe Bwana, iku zote
Tusaidie kwa yote
Mwendo wetu wote vivyo
Uwe kama tuombavyo

Exit mobile version