Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 101 Ewe, Baba wa Mbinguni. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 101 Ewe, Baba wa Mbinguni. Maneno ya wimbo

 

Ewe, Baba wa Mbinguni
Usikie twombalo
Hapa chini duniani
Na uwe radhi nalo

Chorus
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawo wawili

Watu hawa mbele zako
Na mbele ya kanisa
Watimize Neno lako
Wanakutana sasa

Kama Yesu na kanisa
Ni mmoja na hivyo
Watu hawa wape sasa
Wawe mmoja vivyo

Walinde, Bwana, daima
Wabariki nyumbani
Uwape nyingi salama
Humu ulimwenguni

Wabariki, ewe Bwana
Watu hawa wawili
Wape upaji wa wana
Wafurahishwe kweli

Siku zao duniani
Zitakapopungua
Wape kurithi Mbinguni
Mema ya kwendelea

Exit mobile version