Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 95 ZILETENI ZAKA KWA HAZINA nyimbo za wokovu
1
Sikieni neno la Mungu Wetu,
Zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote;
mibaraka itakuja.
Zileteni zaka kwa hazina,
kanijaribu sasa nazo;
Nitakupeni mibaraka,
zaidi ya nafasi ya kupewa.
2
Wataka Roho Mtakatifu kwako?
Uzilete zaka kwa hazina.
Ukae karibu na Bwana wako,
ndipo utabarikiwa.
3
Je, una kasoro na Bwana wako?
Uzilete zaka kwa hazina,
Uzilete kama alivyo sema,
Ndipo utabarikiwa.
4
Ushukuru Bwana na moyo wote,
unapoleta zaka ghalani,
Usadiki ahadi zake zote,
ndipi utabarikiwa.
5
Tuimbe sote nyimbo za furaha,
tunapoleta zaka ghalani,
Twimbe kabisa na furaha kubwa,
kwani tutabarikiwa.