Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 94 PO POTE MASHAMBA YAJAA nyimbo za wokovu
1
Po pote mashamba yajaa,
tele nafaka pevu,
Po pote yang’aa meupe
bondeni na nyandani.
Mwenye mavuno,
twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao,
hata kazi yaishe.
2
Wapeleke uchaoni,
waende na jotoni,
Hata jua lishukapo
wakusanye ko kote.
3
Enyi wakazi wa Bwana
yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake
na furaha kuu.