Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 93 JUA LA ROHONI MWANGU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 93 JUA LA ROHONI MWANGU nyimbo za wokovu

 

1
Jua la rohoni mwangu,
mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana,
Ukiwa karibu Bwana.

2
Nikipata usingizi,
Nijaze fikira hizi,
Ni tamu sana, nilale
pendoni mwako milele.

3
Kaa nami, ewe Bwana,
Usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe;
ni uhai kuwa nawe.

4
Kama mtoto mnyonge
ameshawishwa atange,
Mtafute Ewe Bwana,
ujirudishie tena.

5
Wagonjwa wape amani,
waneemeshe maskini,
Waliao, Mtulizi,
Wape wote usingizi.

6
Asubuhi tutokapo,
tukaribie tulipo;
Twingiapo duniani
tuwe mwako mkononi.

Exit mobile version