Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 92 MAGHARIBI JUA nyimbo za wokovu
1
Magharibini jua
Limekwisha kushuka,
Mwezi na nyota sasa
Vinamsifu Muumba
Wa usiku.
Mungu mtukufu,
Mungu Mkuu,
Wote juu mbinguni,
Na wanadamu chini
Twakusifu.
2
Mpaji wa uhai,
Ukaaye mbinguni.
Utuhifadhi sisi,
Tufahamu gizani,
U Karibu.
3
Mapenzi yako makuu
Yawe nasi usiku,
Tuli usingizini,
Kucha vivyo rohoni
Tushukuru.
4
Na utakapokuja
Na nguvu kutawala,
Mungu wangu kubali
Kunichukua mimi
Uliko juu.
Baba, Mwana, Roho,
Mungu wetu,
Wote juu mbinguni,
Na wanadamu chini
Twakusifu.