Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 90 MAPYA NI MAPENZI HAYO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 90 MAPYA NI MAPENZI HAYO nyimbo za wokovu

 

1
Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tuonayo;
Saa za giza hulindwa,
kwa uzima kuamka.

2
Kila siku, mapya pia,
Rehema, wema, na afya.
Wokovu, na msamaha,
mawazo mema, furaha.

3
Tukijitahidi leo
na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza.

4
Mambo yetu ya dunia
Bwana atayang’aria,
Matata atageuza
yawe kwetu ya Baraka.

5
Yaliyo madogo, haya
Bwana tukimfanyia,
Yatosha tutafaidi
Huvuta kwake zaidi.

6
Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote;
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.

Exit mobile version