Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 85 SALAMA TUMEPITA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 85 SALAMA TUMEPITA nyimbo za wokovu

 

1
Salama tumepita,
Safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi,
Atubariki sasa;
Siku hiyo ya raha,
Siku bora ya juma;
Siku hiyo ya raha,
Siku bora ya juma;

2
Utupe nuru leo
Toka hazina yako;
Ondoa dhambi zetu
Tupokee na pendo;
Mikono yapumzika,
Tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika,
Tuishi ndani yako.

3
Twakusanyika hapa,
Tusifu jina lako;
Ukaribie kwetu,
Tupe neema Bwana
Utamu tusikize
Wa raha ya milele;
Utamu tusikize
Wa raha ya milele;

4
Injili yako leo,
Ishike wenye dhambi;
Itupe nguvu nyingi,
Iponye wenye shida;
Mioyo yetu shangaza,
Vyakula utulishe.
Mioyo yetu shangaza,
Vyakula utulishe.

Exit mobile version