Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 84 IKUMBUKE SABATO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 84 IKUMBUKE SABATO nyimbo za wokovu

 

1
Ikumbuke kote,
Sabato ya Bwana,
Siku tamu na bora,
kupita nyingine;
Yatuletea raha,
na furaha kweli
Mwanga wake hungaza,
urembo wa Yesu.

Karibie, Karibie,
Sabato tamu;
Karibie, Yesu pia,
Bwana wa raha.

2
Itakase kweli,
ukamsifu leo,
Yeye aliyesema,
Mimi ndiye njia
Nasi tukimfuata
Mkombozi hapa.
Atatunywesha tele
maji ya uzima.

3
Siku ya Nderemo!
Tupishe wakati,
Tukimwimbia Yesu
Rafiki Mpendwa;
Mponya wetu leo,
U mwema ajabu!
Ukae kwetu, Bwana,
moyoni daima.

Exit mobile version