Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 82 NI SIKU YA FURAHA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 82 NI SIKU YA FURAHA nyimbo za wokovu

 

1
Ni siku ya furaha,
Ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha,
Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu,
Wadogo, wakubwa;
Hukaribia mbingu,
Lilipo Baraka.

2
Leo, ndiyo bandari,
Nasi twawasili,
Hivyo bustani nzuri,
Ya nyingi fadhili;
Kijito cha baridi
Kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi,
Twanywa maridhawa.

3
Leo ngazi na iwe
Ifikayo juu,
Mawazo na yasiwe
Ya duniani tu;
Leo ni kujilisha
Chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha
Kwa mambo ya Mungu.

Exit mobile version