Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 76 MRITHI UFALME nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 76 MRITHI UFALME nyimbo za wokovu

 

1
Mrithi ufalme, kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka, simama, uvae silaha,
Haraka sana, saa zapita.

2
Mrithi ufalme mbona ‘kawia?’
M-bona hupokei zawadi?
Haya, uvae, Mwokozi yuaja;
Haraka, umlaki afikapo.

3
Mataifa makuu ya dunia
Yapigana na kujiangusha.
Usizihofu dalili, mrithi;
Ishara zote hazikawii.

4
‘Sitazame anasa za dunia!
Kwani hayo yapita upesi.
Zivunje kamba zinazokufunga.
Mrithi ufalme, njoo ‘karudi.

5
Inua kichwa, tazama mbele tu,
M-falme aja na utukufu;
Jua laonekana milimani,
Warithi ufalme furahini.

Exit mobile version