Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 72 JENGA JUU YA MWAMBA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 72 JENGA JUU YA MWAMBA nyimbo za wokovu

 

1
Tutajenga juu ya mwamba
Wa Yesu, Mwamba wa kale;
Tutavumilia kishindo
tufani ivumapo.

Tutajenga juu,
(tutajenga juu ya mwamba mkuu)
Tutajenga juu,
(tutajenga juu ya mwamba mkuu)
Tutajenga juu ya mwamba mkuu,
juu yake Yesu.

2
Wengine hujenga katika
Mchanga wa ulimwengu;
Wengine katika mawimbi
Ya anasa za dhambi.

3
Jenga nawe juu ya mwamba,
Msingi pekee wa kweli;
Tumai lake litadumu,
Tumai la wokovu.

Exit mobile version