Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 71 KESHENI KAOMBENI nyimbo za wokovu
1
Kesha, ukaombe
Panapo nafasi;
Wakati si mwingi,
Kwa vile ukeshe.
Mwili ni dhaifu,
Adui hodari;
Karibu atakuja,
Bwana wa Arusi.
Kesha, Omba,
Kesha, Omba,
Kesha kaombe gizani,
Mchana,
Daima kesha.
2
Fukuza usingizi,
Fukuza mashaka;
Ahadi ni yako,
Raha ya milele.
Bwana alikesha
Kwa ajili yako;
Jasho lake likawa
Matone ya damu.
3
Yesu umkubali
Awe nguvu zako;
Silaha uzivae;
Adui karibu.
Sasa nafasi iko,
Isipite bure;
Bila kukawia
Masihiya kesha.