Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 69 CHA KUTUMAINI SINA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 69 CHA KUTUMAINI SINA nyimbo za wokovu

 

1
Cha kutumaini sina
ila damu yake Bwana,
Sina wema wakutosha,
Dhambi zangu kuziosha.

Kwake Yesu nasimama,
Ndiye Mwamba; ni salama;
Ndiye Mwamba; ni salama.

2
Njia yangu iwe ndefu
yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga
nguvu zake ndiyo nanga.

3
Damu yake na sadaka
nategemea daima,
Yote chini yakiisha
Mwokozi atanitosha.

4
Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake
sina hofu mbele zake.

Exit mobile version