Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 65 TWENDENI ASKARI nyimbo za wokovu
1
Twendeni askari
Watu wa Mungu,
Yesu yuko mbele,
Tumwandame juu;
Ametangulia
Bwana vitani,
Twende mbele
Kwani ndiye amini.
Twendeni askari
Watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele,
Tumwandame juu.
2
Jeshi la shetani,
Likisikia
Jina la Mwokozi,
Litakimbia;
Kelele za shangwe
Zivume pote;
Ndugu, inueni
Zenu sauti.
3
Kweli kundi dogo,
Watu wa Mungu.
La mababa yetu
Ni Letu fungu,
Hatutengwi nao,
Moja imani,
Tumaini moja,
Na moja dini.
4
Haya mbele watu
Nasi njiani,
Inueni mioyo,
Nanyi sifuni;
Heshima na sifa
Yake Mfalme,
Juu hata chini
Sana zivume.