Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 61 BWANA NAMI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 61 BWANA NAMI nyimbo za wokovu

 

1
Nimemwona rafiki
Wa thamani kubwa,
Ananipenda kwa ‘pole,
Kwa pendo amini
Kuishi kutengwa naye,
La, huku siwezi,
Tunakaa pamoja:
Bwana nami.

2
Pengine ninachoka
Mimi mdhaifu,
Ndipo ninamtegemea
Alivyoalika;
Huniongoza njiani
Pahali pa nuru,
Twatembea pamoja
Bwana nami.

3
Namweleza huzuni
Na furaha yangu
Vile vinavyosumbua,
Vinavyopendeza;
Huniagiza kutenda
Yanayonipasa,
Twazungumza pamoja;
Bwana nami.

4
Ajua natamani
Kuwavuta watu,
Hivyo ananipeleka
Kutangaza Neno;
Nitangaze pendo lake,
Kwa nini akafa;
Twahubiri pamoja;
Bwana nami.

Exit mobile version