Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 57 USIKATAE KAZI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 57 USIKATAE KAZI nyimbo za wokovu

 

1
Usiikatae
Kazi yake Bwana;
Ukae tayari
Kuifanya kazi;
Uende po pote
Mungu akwitapo,
Nawe utaona
Furaha Kazini.

Njoo, we!
Usiikatae;
Njoo, we!
Uifanye kazi;
Usikatae
Kazi yake Bwana,
Ili hatimaye
Usikatazwe juu.

2
Usiikatae
Kazi yake Bwana,
Kwa nini kawia?
Fanya kazi leo.
Mavuno meupe,
Wachache wavuni,
Onyesha furaha
Kwa kazi ya Bwana.

3
Usiikatae
Kazi yake Bwana,
Kukataa pendo
Kwako ni hatari.
Saa ya rehema,
Yesu akiomba,
Ziungame dhambi,
Zifutwe mbinguni.

Exit mobile version